Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amefichua kuwa bodi ya klabu hiyo ilipiga kura ya kupinga kumsajili Cristiano Ronaldo msimu huu wa joto. (Bild via Mail)
Fowadi huyo wa Ureno alipoiambia Manchester United kwamba alitaka kuondoka Old Trafford mwanzoni mwa Julai, Bayern ilitangazwa kwa haraka kama klabu inayopendekezwa kuwa klabu yake inayofuata.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Bundesliga hivi karibuni walijiondoa kwenye dili, sawa na Chelsea na Atletico Madrid.
Everton wameiomba Chelsea kumjumuisha kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 22, au mchezaji wa kimataifa wa Albania Armando Broja, 20, kwa mkopo kama sehemu ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji Anthony Gordon, 21. (talkSPORT)
Toffees hatimaye wako tayari kumuuza Gordon ikiwa wanaweza kupata mbadala inayofaa. Mshambulizi wa Watford Mbrazil Joao Pedro, 20, na mchezaji wa kimataifa wa Southampton na Scotland Che Adams, 26, ni miongoni mwa wachezaji ambao klabu hiyo imewaulizia. (Mirror)
Gordon ameiambia Everton kuwa anataka kusainiwa na Chelsea ili kucheza soka ya Ligi ya Mabingwa na kuongeza nafasi yake ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha England cha Kombe la Dunia. (Athletic – subscription required)

CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA
Manchester United bado wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, licha ya kuwasili kwa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 30, kutoka Real Madrid. (Mirror)
United wanataka kumpa mlinda mlango wa Eintracht Frankfurt na Ujerumani Kevin Trapp, 32, mshahara wa kila mwaka wa takriban euro milioni 10-11 (£8m-£9m) ili kujiunga na klabu hiyo.. (Sport1 – in German)
Ofa mpya kwa mshambuliaji wa Ajax Antony, 22, inatarajiwa kuwasilishwa na United huku klabu hiyo ikishinikiza kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Gianluigi Longari via Twitter)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
West Ham wamewasilisha dau jipya la euro milioni 11 pamoja na nyongeza kwa kiungo wa Club Bruges na Ubelgiji Hans Vanaken, 29. (Fabrizio Romano via Twitter)
Miamba ya Italia Roma na Inter Milan zote zina nia ya kumsajili mlinzi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Muingereza Trevoh Chalobah kwa mkopo. (90min)
Nottingham Forest haiko karibu kufikia makubaliano ya mlinzi wa Tottenham Muingereza Japhet Tanganga, huku AC Milan wakisalia kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Fabrizio Romano via Twitter)
Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin mwenye umri wa miaka 27 kutoka Uhispania. (Sport)
