Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 67 kwa kiungo wa kati wa Real Madrid Casemiro, 30 na mara mbili ya mshahara wa Mbrazil huyo hadi £360,000 kwa wiki, baada ya mazungumzo na kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 27, kuvunjika. . (Relevo – in Spanish)
Lakini sasa dili la Casemiro inasemekana kuwa haiwezekani kwa United, huku mchezaji huyo akisemekana hataki kuhama na Chelsea pia ikionyesha nia. (Talksport)
United pia wanafikiria kumsajili beki wa kulia wa Ubelgiji Thomas Meunier, 30, kutoka Borussia Dortmund kama watamuuza beki wa pembeni wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 24, kurudi Crystal Palace kwa £10m. (Telegraph – subscription required)
The Red Devils wanajipanga kumnunua mlinda lango wa kimataifa wa Uswizi wa Borussia Monchengladbach Yann Sommer, 33, ili kumpa changamoto David de Gea. (Blick, via Sun)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Sporting Lisbon wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amewaambia mara kwa mara Manchester United kwamba anataka kuondoka. (90min)
Willian anaweza kurejea Ligi ya Premia kwani ripoti zinaonyesha yuko tayari kuanza mazungumzo na Fulham, winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 34 hivi karibuni aliondoka Corinthians na anaweza kusajiliwa bila malipo. (Mail)
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang angependelea kuondoka Barcelona na kwenda Chelsea kuliko Manchester United, kulingana na ripoti ambazo pia zinaonyesha kwamba Barcelona wanamthamini kwa pauni milioni 25, kiasi ambacho Chelsea inasita kumlipa mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon, 33. (Telegraph, via Express)
Tottenham wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ukraine Ruslan Malinovskyi kutoka Atalanta, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa wa nane kusajiliwa na Spurs katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (TuttoAtalanta – In Italian)
Southampton na Newcastle zote zinataka kumsajili mshambuliaji wa Benfica Goncalo Ramos, 21, wa Ureno. (Telegraph – subscription required)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Liverpool na Guinea Naby Keita, 27, anaweza kuwa tayari kuondoka, huku klabu ya zamani ya RB Leipzig ikionyesha nia. (Sky Sports Germany)
Lakini inafahamika kuwa Liverpool hawana nia ya kumwachia Keita kabla ya mwisho wa dirisha hili la usajili na wanatumai kumfanya asaini kandarasi mpya, ingawa wanaweza kuhatarisha kumwacha huru msimu ujao. (Goal)
West Ham wameachana na nia yao ya kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emerson, 28, kutokana na madai ya mshahara mkubwa wa Mbrazil huyo. (Guardian)
CHANZO: BBC SWAHILI