
Chelsea wameanza mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati Mholanzi Frenkie de Jong, 25, ambaye amekuwa akihusishwa pakubwa na Manchester United msimu huu. De Jong angependelea kuhamia Chelsea badala ya Manchester United.
–
Chelsea wako tayari kumpa beki Mfaransa Wesley Fofana pauni 200,000 kwa wiki kama wanaweza kufanya makubaliano na Leicester City, ambao wanataka pauni milioni 85 kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Manchester United wamefanya mazungumzo ya mapema na RB Salzburg kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Slovenia mwenye umri wa miaka 19 Benjamin Sesko. Chelsea pia imekuwa na mkutano na wakala wa Sesko.
–
Bournemouth wanakaribia kumsajili kipa wa Barcelona mwenye umri wa miaka 33 Neto kutoka Brazil.

Kipa wa England Dean Henderson, 25, hataichezea Manchester United tena baada ya kujiunga na Nottingham Forest kwa mkopo, kulingana na kiungo wa zamani wa Tottenham Jamie O’Hara.
–
Mlinzi wa Chelsea Mwingereza Levi Colwill, 19, anatazamiwa kujiunga na Brighton, huku mlinzi wa The Seagulls Mhispania Marc Cucurella, 24, akikaribia kuhamia Chelsea. The Blues watakuwa na kipengele cha kumnunua Colwill katika mkataba huo.

Tottenham wameanza mazungumzo na Udinese kuhusu beki wa kushoto wa Italia Destiny Udogie, 19, na uwezekano wa kumuuza kwa mkopo beki huyo katika klabu hiyo ya Serie A.
–
Winga wa Croatia Ivan Perisic, 33, aliwasiliana na nyota wa zamani wa Tottenham na mshirika mwenzake Luka Modric kwa ushauri kabla ya kuamua kuondoka Inter Milan kuelekea London kaskazini msimu huu.
–
Vilabu kadhaa vya Championship na League One vina nia ya kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Wales Charlie Savage, 19.