Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20.08.2022

Chelsea wametoa ofa ya pauni milioni 15 pamoja na beki wa Uhispania Marcos Alonso, 31, kwa mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 33 kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.
–
Mwenyekiti wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amekanusha uvumi unaohusisha klabu hiyo ya Bundesliga na mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anasema hakuna mawasiliano yoyote na nyota huyo wa Manchester United.
–
Beki wa Leicester Mfaransa Wesley Fofana, 21, ameomba kutohusika watakapokabiliana na Southampton wikendi hii baada ya kuhusishwa na Chelsea.

Manchester United wamefikia makubaliano na Real Madrid kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Casemiro kwa dau la hadi £70m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa na Real tangu 2013, akishinda mataji matatu ya La Liga na matano ya Ligi ya Mabingwa.
–
Nice ya Ufaransa iko kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 27.
–
Real Madrid wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Hotspur na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, kuchukua nafasi ya Mbrazili anayeondoka Casemiro, 30, ambaye amekubali mkataba na Manchester United.
–
Newcastle na West Ham wanatazama matukio katika United kwa karibu, wote wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa Scotland Scott McTominay, 25, kwa kuwa wanaamini kuwa ndiye kiungo anayewezekana kutengwa na ujio wa Casemiro.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ana imani kuwa winga wa Uingereza Bukayo Saka, 20, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo licha ya wapinzani, wakiwemo Manchester City, kuonyesha nia.
–
Everton wako tayari kumsajili Mohammed Kudus kwa mkopo kutoka Ajax kwa nia ya kufanya uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Ghana, 22, kuwa wa kudumu.
–
Leeds wanalenga kukamilisha dili la kumnunua Willy Gnonto, 18, wa FC Zurich, kwa £4m huku mshambuliaji huyo wa Kiitaliano akiingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake.

Ajax pia wanataka kumrejesha kiungo wa Morocco Hakim Ziyech, 29, kutoka Chelsea ikiwa Mbrazil Antony, 22, atajiunga na Manchester United. .
–
Antony alifanya mazoezi peke yake siku ya Ijumaa baada ya klabu hiyo ya Uholanzi kukataa ofa ya pauni milioni 67 kutoka kwa United.
–
Chelsea wameuliza kuhusu kupatikana kwa mlinzi wa Manchester United na England Harry Maguire, 29, kwa ajili ya makubaliano ya kubadilishana ambayo yatamfanya mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 23, kwenda upande wa pili.