
Chelsea wana imani kuwa wanaweza kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Everton Anthony Gordon, 21, wiki hii huku mazungumzo kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 21 yakiendelea.
–
Manchester United wako tayari kukamilisha usajili wa fowadi wa Ajax Antony, 22, ndani ya wiki ijayo, baada ya kuripotiwa kuafikiana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.
–
Chelsea wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang, 33, kwa mkataba unaodhaniwa kuwa wa thamani ya kati ya £15m na £25m.

The Blues wako tayari kuruhusu wachezaji wanane wa ziada kuondoka katika dirisha hili baada ya West Ham kukubali dili la kumsajili beki wa Italia Emerson Palmieri, 28.
–
Maafisa kutoka Manchester United wanatazamiwa kusafiri hadi Barcelona katika juhudi za mwisho za kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
–
United pia wanavutiwa na mlinda mlango wa Eintracht Frankfurt na Ujerumani Kevin Trapp, 32.

Watford “haitawasilisha ombi lolote” kwa mshambuliaji wa Senegal Ismaila Sarr na wako tayari kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mkataba mpya wa muda mrefu baada ya pendekezo lake la kuhamia Aston Villa kushindwa.
–
The Hornets pia hawajakubali ofa ya Newcastle United ya £25m kwa fowadi wa Brazil Joao Pedro. Magpies watahitaji kuongeza ombi lao kwa kijana huyo wa miaka 20.
–
Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Leeds na Wales Daniel James, 24

Barcelona wanamtazama beki wa kushoto wa Celta Vigo Mhispania Javi Galan, 27, kama mbadala wa mlinzi wa Chelsea Marcos Alonso kwa sababu uhamisho wa klabu hiyo ya Catalan kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, 31 unazidi kuwa mgumu.
–
Wolves wamekubaliana masharti ya kibinafsi na mshambuliaji wa VfB Stuttgart na Austria Sasa Kalajdzic lakini mazungumzo kati ya klabu hizo mbili bado yanaendelea kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka ada ya juu zaidi ya uhamisho.