
Manchester United wamewasiliana na Bayern Munich kuhusu uwepo wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Leroy Sane, 26. Liverpool pia wana nia ya kuwasilisha ombi kwa winga huyo wa Ujerumani.
–
Chelsea wametoa euro 70m (£59m), pamoja na beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso, 31, kwa lengo la kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25.

Tayari makubaliano yamefikiwa kwa masharti ya kibinafsi kati ya Barca na Alonso.
–
Manchester United inaweza kumpeana kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 25, katika makubaliano ya kubadilishana na De Jong. United pia inamtazama kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 26, kama mbadala wa De Jong.

Bournemouth wako tayari kumsajili beki wa kati wa Feyenoord na Argentina Marcos Senesi, 25.
–
Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg kutoka Slovenia Benjamin Sesko, 19, ameamua kusalia na klabu hiyo ya Austria msimu huu licha ya Chelsea na Manchester United kumtaka.
–
Wakala wa Sesko pia amefanya mazungumzo na mkurugenzi wa RB Leipzig kuhusu uwezekano wa kuhamia Ujerumani.

Manchester United wamemuongeza winga wa Uholanzi na mchezaji bora wa mwaka wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, kwenye orodha yao ya uhamisho kutoka PSV Eindhoven. Mkufunzi wa United Erik ten Hag ana jukumu kubwa katika harakati za klabu hiyo kutafuta kipa wa pili nyuma ya David de Gea kufuatia uhamisho wa mkopo wa Dean Henderson kwenda Nottingham Forest.
–
Mmiliki mpya wa Chelsea Todd Boehly alimsafirisha beki wa kushoto wa Uhispania Marc Cucurella, 24, hadi Mykonos nchini Ugiriki ili kukamilisha uhamisho wake kutoka Brighton.