
Leicester na Southampton ziko macho baada ya winga Muingereza Callum Hudson-Odoi, 21, kuomba kuondoka Chelsea kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Borussia Dortmund pia wana nia ya kutaka kumnunua Hudson-Odoi.
–
Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, anakaribia kurejea RB Leipzig.

Villarreal wana uhakika wa kumchukua kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso, 26, kutoka Tottenham kwa mkataba wa kudumu baada ya kufanikiwa kwa mkopo msimu uliopita.
–
Mkurugenzi wa spoti wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amepuuza mapendekezo kwamba Manchester United imefanya uchunguzi kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Leroy Sane, 26.

United bado inaendelea kufanyia kazi mkataba wa mshambuliaji wa Slovenia mwenye umri wa miaka 19 Benjamin Sesko kutoka Red Bull Salzburg.
–
Newcastle pia wako tayari kushinikiza kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia anayekadiriwa kuwa bora.

Wolves imekataa ofa ya mkopo kutoka kwa klabu ya Italia ambayo haijatajwa jina kwa ajili ya mlinzi wao Mreno Toti Gomes, 23.

Kiungo wa kati wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, 24, ameongeza mkataba wake na PSV Eindhoven hadi 2027, licha ya West Ham kumtaka.
–
Mlinzi wa Argentina Marcos Senesi, 25, anatarajiwa kuhamia Bournemouth kutoka Feyenoord kwa pauni milioni 12.6.