Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 15.08.2022

Cristiano Ronaldo alipewa ofa na Manchester United kwa wapinzani wao AC Milan na Inter Milan, lakini klabu zote za Serie A zilikataa nafasi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37.

Pierre-Emerick Aubameyang anataka kupigania nafasi yake katika klabu ya Barcelona, ambayo imekataa dau la £12m (€14m) kutoka kwa Chelsea kumnunua mshambuliaji huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 33.
–
Barcelona wanataka ada ya pauni milioni 23 (€28m) kwa Aubameyang, ambaye alijiunga nao kwa uhamisho wa bila malipo mwezi Februari.
–
Wakati huo huo, meneja Xavi ameiomba Barcelona kumsajili tena mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, kutoka Paris St-Germain.
–
Manchester United imejiunga na orodha ya vilabu vya Premier League, vikiwemo Arsenal na West Ham, vinavyotaka kumsajili kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo, 20, kutoka Brighton.
–
Nottingham Forest wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 24, ambaye hapo awali amekuwa akihusishwa na Arsenal. Forest pia wamewasilisha dau la pauni milioni 17 kwa kiungo wa Eintracht Frankfurt na Uswizi Djibril Sow, 25.

Leicester City wako tayari kuruhusu Arsenal kumsaka kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, kuondoka bila malipo msimu ujao.
–
Everton wametoa ofa kwa mshambuliaji wa Rennes wa Guinea, Serhou Guirassy, 26.
–
Blackburn inaongoza harakati za kumsajili beki wa kati wa Uholanzi Sepp van den Berg, 20, kwa mkopo kutoka Liverpool. Mkataba uliopendekezwa unajumuisha kipengele cha adhabu ikiwa beki huyo hatacheza mechi za kutosha kwa upande wa Ubingwa.

Nice wameuliza kuhusu beki wa kushoto wa Chelsea wa Brazil Emerson Palmieri, 28.
–
Brighton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kushoto wa Villarreal Pervis Estupinan, 24.
–
Everton wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Villarreal na Senegal Nicolas Jackson, 21, kwa kuanzisha kipengele chake cha kuachiliwa kwa pauni milioni 27. Bournemouth wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Ghana Abdul Mumin, 24, kutoka Guimaraes.