ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
July mwaka 1991 huko Detroit nchini Marekani kulitokea tukio liloacha wengi vinywa wazi baada ya mwanaume mmoja aliefahamika kwa jina la Gregory green kumshambulia kwa visu mkewe Thonya green aliekuwa mjamzito paka kufa.
–
Tonya alimvumilia sana Gregory kwa tabia ya kumpiga mara kwa mara. Lakini uvumilivu wake ndio uliosababisha kifo chake. Akiwa mjamzito wa miezi sita walipishana maneno na mumewe.
–
Gregory alimkamata mkewe na kumpiga visu vya tumbo zaida ya vitatu bila kujali kuwa mkewe ni mjamzito. Kilichofata Tonya alifariki kwa kupoteza damu nyingi huku akikimbizwa hospital na majirani.
–
Mwanaume yoyote anaekupiga huyo hana mapenzi na wewe na ukifanya mchezo kuna siku atakuua. Mapenzi ni kuvumiliana na kuelekezana kwenye kasoro nasi kupigana. Usikubali kuishi na mwanaume anaekupiga.
–
Imeandikwa na Abdulrazaki issa.