Wakenya wanasubiri rais mteule William Ruto kuapishwa rasmi ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi huku viongozi wa mataifa mbalimbali wanaendelea kumpongeza na kumtakia mema.
–
Kwa mujibu wa katiba,rais mteule anapaswa kuapishwa Jumanne ya kwanza inayoangukia kipindi cha wiki mbili baada ya kutangazwa rasmi iwapo hakuna kesi yoyote ya kupinga matokeo inayowasilishwa kwenye mahakama ya juu kabisa ya nchi.
–
Endapo kesi yoyote inawasilishwa,rais mteule ataapishwa siku ya saba baada ya mahakama ya juu kuitoa uamuzi wake.
–
Kufikia sasa hakuna aliyewasilisha kesi mahakamani. Akitoa tathmini yao ya uchaguzi, mwenyekiti wa ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete amesisitiza juu ya umuhimu wa kuufuata mchakato wa sheria.
–
Walalamishi wana muda wa wiki moja kuwasilisha kesi mahakamani.
–
Credit – DW