Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime amesema wale wote waliohusika na uhalifu wa vishwambi vya sensa kwenye maeneo yaliyoripotiwa ya Arusha na Katavi, kuviwasilisha vifaa hivyo haraka iwezekanavyo kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa kwa waliohusika.
–
Hata hivyo, ametoa wito kwa makalani wa Sensa ambao wanaendelea na zoezi hilo muhimu kwa taifa kuwa makini na vifaa hivyo kwani kutokana na uchunguzi imeonekana kuna uzembe unaofanywa na baadhi ya makalani na kuwataka makalani hao kuendelea kuzingatia mafunzo/maelekezo waliyopewa.
–
Aidha, hadi sasa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaendelea vizuri kwenye maeneo yote nchini.