Wakazi wa Ndindiruku kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya, baadhi ya wakazi wamelazimika kuwazika wapendwa wao kwa magunia kutokana na gharama kubwa za mazishi.
“Tunanunua gunia kwa Ksh50 [takribani TZS 1,000] pekee na kumzika mtu huyo, na inatuchukua dakika 20 pekee,” amesema mmoja wa wakazi hao.
Katika kisa kilichotokea hivi karibuni, wakazi wa kijiji hicho waliamua kwenda kumzika mpendwa wao kwa gunia kabla ya kiongozi wa eneo hilo kuingilia kati na kununua jeneza.
Credit – Swahili Times