ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Thursday, October 5, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

WAZIRI MKUU AUNGANA NA MAMIA KUMUAGA MREMA

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Aug 24, 2022
in HABARI
0
WAZIRI MKUU AUNGANA NA MAMIA KUMUAGA MREMA
0
SHARES
190
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

SERIKALI KUTUMIA GESI ILI KUZALISHA UMEME NCHINI

SERIKALI KUTUMIA GESI ILI KUZALISHA UMEME NCHINI

Oct 4, 2023

RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA NCHI KAVU WA INDIA

Oct 4, 2023

WANAFUNZI 8,000 WA STASHAHADA KUPATA MKOPO WA ELIMU

Oct 4, 2023
Load More

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kumkumbuka Mhe. Augustino Lyatonga Mrema kutokana na mchango wake mkubwa wa kuendeleza mahusiano na vyama vya siasa.

“Mheshimiwa Mrema atakumbukwa kama kiongozi mkuu wa Chama cha TLP kwa muda mrefu sana. Na akiwa katika siasa, aliisaidia Serikali kupata mwelekeo mzuri wa vyama vya siasa,” amesema Waziri Mkuu.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Agosti 24, 2022) wakati akizungumza na mamia ya waombolezaji kwenye ibada ya kumuaga marehemu Mrema katika Parokia ya Mt. Augustino Kilimahewa, Salasala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

 

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, kwenye Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

.

Amesema salamu za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ziliwasilishwa asubuhi na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

“Sisi tuliopo hapa tuna mambo mawili makubwa ya kufanya ili kumuenzi ndugu yetu Mrema. Moja ni kuenzi yale yote aliyofanya kwa upande wa Serikali na upande wa siasa lakini pili, tuendelee kumuombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuilaza roho yake mahali pema peponi,” amesema.

Kuhusu mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi huko Kiraracha, Moshi, Waziri Mkuu amesema Serikali itawakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohudhuria ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Akizungumza na niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo, DCP Anthony Luta alisema Jeshi la Polisi litaendelea kumkumbuka Mhe. Mrema kwa mambo kadhaa ikiwemo hatua yake ya kuanzisha jeshi la ulinzi wa sungusungu, ujenzi wa vituo vidogo vya polisi na utetezi wa haki za wanawake ambapo kwa sasa wameanzisha madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi.

Naye Paroko wa kanisa hilo, Padre Peter Assenga alisema Mhe. Mrema alikuwa akijitolea kwa mambo mengi parokiani hapo na ataendelea kukumbukwa sana.

 

 

Wafiwa na Viongozi wa Siasa wakiwa katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu alisema umati mkubwa uliokuwepo kanisani hapo ni ishara tosha ya jinsi Bw. Mrema alivyoishi vizuri na watu wakiwemo viongozi wa Serikali na vyama vya siasa.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu mmoja na mapadre sita. Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Hamad Rashid, Prof. Ibrahim Lipumba, John Cheyo, Steven Wassira, James Mbatia, Joseph Selasini na Mchungaji Dkt. Eliona Kimaro.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, baada ya ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema, iliyofanyika katika Kanisa la Roman Catholic Salasala, jijini Dar es Salaam, Agosti 24 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Related

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

SERIKALI KUTUMIA GESI ILI KUZALISHA UMEME NCHINI
HABARI

SERIKALI KUTUMIA GESI ILI KUZALISHA UMEME NCHINI

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023
RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA NCHI KAVU WA INDIA
HABARI

RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA NCHI KAVU WA INDIA

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023
WANAFUNZI 8,000 WA STASHAHADA KUPATA MKOPO WA ELIMU
HABARI

WANAFUNZI 8,000 WA STASHAHADA KUPATA MKOPO WA ELIMU

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023
‘KUWE NA MIKAKATI MADHUBUTI KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO’
HABARI

‘KUWE NA MIKAKATI MADHUBUTI KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO’

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023
TET YAWASILISHA RASIMU ZA MITAALA MIPYA KWA MAAFISA ELIMU NCHINI
HABARI

TET YAWASILISHA RASIMU ZA MITAALA MIPYA KWA MAAFISA ELIMU NCHINI

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023
BEI Y MAFUTA YAPANDA TENA NCHINI
BIASHARA

BEI Y MAFUTA YAPANDA TENA NCHINI

by SUZO SHUKRANI
Oct 4, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Jul   Sep »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In