Mgombea wa Urais kupitia Chama cha UDA nchini Kenya William Ruto ndiye ameshinda nafasi ya Rais katika Uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo.
Ruto ameibuka mshindi baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Raila Amollo Odinga wa Muungano wa Azimio baada ya kupata kura 7,176,141 dhidi ya mpinzani wake mkuu aliyepata 6,942930.
Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa Bomas , mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati amesema kwamba Ruto amejipatia asilimia 50.49 ya kura naye Raila akaijipatia asilimia 48.85

Source: BBC SWAHILI