ADVERTISEMENT
Mabingwa wa soka Tanzania, klabu ya Yanga wanatarajiwa kucheza na mabingwa wa soka Uganda, klabu ya Vipers.
Mjumbe wa kamati ya kuratibu wiki ya wananchi Taji Lihundi amewaambia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya wananchi kuwa, siku ya kilele cha wiki hiyo klabu ya Yanga itacheza na mabingwa wenzao (Vipers).
Wiki ya wananchi imezunduliwa rasmi hii leo na itafikia kilele chake Agosti 6 mwaka huu katika dimba la Mkapa mkoani Dar es Salaam.
ADVERTISEMENT