Afisa habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally ashusha tambo za pira birianidhidi ya Nyasa Big Bullets kwa mchezo unaofuata kuwa klabu ya Simba haikai kizembe ikichezea nyumbani hivyo wapinzani wake wanabidi kujipanga veyema.
“Tukiwa nyumbani hatuingii kizembe, lazima wapinzani wajue kwamba wamefika Tanzania, wapo nyumbani kwa Mnyama. Tutafanya balaa kubwa zaidi. Hatujamalizaaaa.”- Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally akiongea na Wanasimba kwenye Tawi la Mpira Pesa lililopo Magomeni Mikumi.