Msanii Burna Boy na Tems kutokea kipande cha Nigeria wametajwa kwenye orodha ya wanaowania tuzo katika BET Hip-Hop Awards zitakazofanyika Ijumaa, Septemba 30, 2022, mjini Atlanta, Marekani.
–
Burna Boy yupo kwenye kipengele cha Video Director of the Year baada ya kuongoza video yake ya ‘Last Last’ na Tems yupo kwenye vipengele vitatu ‘Best hip hop video, Best collaboration na Song of the year’ kutokana na colabo na Future ‘Wait For U’.