Benki ya NBC imechangia pakti 3000 za taulo za kike kupitia kampeni ya Namthamini inayo endeshwa na East Africa TV, ambazo zitaweza kuwasaidia watoto wa kike 250 kwa kipindi cha mwaka mzima.
Hii ikiwa ni moja kati ya michango mbali mbali ambayo Benki ya NBC inaendelea kutoa kwa jamii kupitia sekta ya elimu, afya, n.k
Akikabidhi mchango huo kwa Mratibu wa Kampeni ya Namthamini Bi. Nancy Mwanyika (wa pili kulia) ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Bi. Irene Peter (wa pili kushoto).
Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Bi. Najma Paul na Bw. Justine Kessy, watendaji wa EATV na East Africa Radio.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT