Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa Benki ya NBC Bw. Abel Kaseko, Mkuu wa Kanda Bi. Zubeida Haroun na Meneja Tawi Sumbawanga Bw. Mukiza Aggrey kwa pamoja katika kutimiza dhana y benki hiyo kuwa karibu na jamii inayoizunguka na kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye sekta ya elimu, inayo furaha kuchangia madawati 30 kwa wilaya ya Sumbawanga.
Dhumuni la msaada huu ni kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma kwenye wilaya hiyo. Msaada huo ulipokelewa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Sebastian Waryuba .

