
Benki ya NMB yaibuka kinara kwa kutunukiwa Tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara Tanzania 2022 kutoka Jarida la Global Banking and Finance la jijini London, Uingereza.
Benki hio imeamua kuielekeza Tuzo hio kwa wateja na wadau wake kwa kuendelea kutuamini na kuwa sehemu ya mafanikio yake. Imeongeza kwa kuahidi kuendelea kuwapa huduma bora zinazokidhi mahitaji yao ya kifedha.
