Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro imemuhukumu Bibi Monica Mgaza(70) kutumikia kifungo cha mika nane gerezani wakati Abdalla Idd na Rajabu Omary nao wakihukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja kwa kosa la kumuua bila kukusudia Samwel Ngilwa ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa namba moja Bibi Monica Mgaza.
–
Akisoma hukumu hiyo Septemba 16, 2022 Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro Masseka Chaba, amesema mahakama hiyo imewakuta na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mawakili upande wa serikali ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wenyewe kutenda kosa la kukiri kuua bila kukusudia.
–
Jaji Chaba amesema washitakiwa hao, walitenda tukio hilo Februari 27,2017 baada ya marehemu kukutwa amekufa katika mashamba ya mikonge yaliyopo katika kijiji cha Rudewa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
–
Aidha Jaji Chaba amesema washitakiwa hao wamekaa mahabusu kwa mda wa miaka mitano tangu walipokamatwa Februari 2017 hadi sasa 2022.
–
Nje ya mahakama jopo la mawakili wa upande wa utetezi wakiwakilishwa na Abdulla Bwaga, amesema wameridhika na uamuzi wa kesi hiyo namba 32 ya mwaka 2020 kwa kuwa washitakiwa wamekiri kuhusika kutenda kosa hilo la kuua bila kukusudiwa.