Chelsea imemfuta kazi Damian Willoughby mwezi mmoja baada ya kumteua kama mkurugenzi wa biashara, kufuatia shutuma na ushahidi wa unyanyasaji wa kijinsia.
–
Ujumbe wa maandishi kutoka kwa Willoughby uliotumwa kwa wakala wa fedha wa soka wa kike Catalina Kim ulibainika kuwa siyo ‘ujumbe unaofaa’ kwa wakala huyo.
–
Kauli ya Chelsea imeweka wazi kuwa ingawa tukio hilo lilitokea kabla ya kuajiriwa kwa Willoughby, ni wazi sio jambo ambalo litavumiliwa.