Klabu ya Mpira wa Miguu ya COASTAL UNION inautaarifu umma kuwa haina taarifa rasmi kutoka kwa KOCHA JUMA MGUNDA wala mawasiliano yeyote ramsi na klabu ya Simba juu ya kujiunga kwake na KLABU YA SIMBA.
Uongozi wa Coastal Union ulikuwa ukiendelea na mazungumzo na Kocha Juma Mgunda kwa ajili ya kuongeza muda wa kuifundisha timu yetu baada ya mkataba wake wa awali kuisha, hivyo suala la Kocha Juma Mgunda na klabu ya Simba ni suala lake binafsi.
Uongozi wa klabu ya COASTAL UNION unapenda kuwajulisha wapenzi wa COASTAL UNION kuwa katika kipindi hiki cha mpito Timu yetu itakuwa chini ya MWALIMU JOSEPH LAZARO (kocha msaidizi wa COASTAL UNION).
COASTAL UNION inawaomba wapenzi wote wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu wa tarehe 10-SEPTEMBA-2022 dhidi ya POLISI TANZANIA uwanja wa MKWAKWANI TANGA.