Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B visiwani Zanzibar, Hamida Mussa Khamis ameingilia kati sakata la majirani wawili walioingia kwenye mgogoro mkubwa kuhusu ujenzi wa fensi za nyumba zao.
Picha za ujenzi wa uzio mbele ya geti la nyumba nyingine, zimeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mkuu huyo wa wilaya kufika eneo la tukio.
Amesema uzembe wa watumishi wa serikali ndiyo uliosababisha tukio hilo kwa watumishi hao kutoa vibali vya ujenzi bila kufika katika maeneo husika.
Credit: Habari Wilaya Magharibi B