Mechi ya ushindani iliyochezwa kati ya klabu ya Azam na Yanga Agosti 6, 2022 ambayo imehusisha sare ya goli 2-2 katika michuano ya kuwania kombe la Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara, imeonekana kuwa ni miongoni mwa Derby bora iliyovutia wengi hapa nchini kama ilivyo Kariakoo Derby inayohusisha Klabu ya Simba na Yanga.