Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally (Semaji kuu la CAF) kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hio ameeleza kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju, Manispaa ya Kinondoni kwamba, kwa sasa unajengewa ukuta (Uzio) wa kuzunguka eneo zima la uwanja huo ili eneo lote lihusikanalo na umiliki wa klabu hio liwe ndani, hio ni baada ya kupata kibali cha kuendelea na ujenzi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh, Amos Makalla kulingana na uwepo wa wavamizi waliojenga kihorera katika baadhi ya sehemu zinazozunguka uwanja bila idhini kutoka kwa kurugenzi ya klabu hio.