
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mags Gaynor ambaye ni Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo katika Ubalozi huo.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa Masuala muhimu hususani eneo la Ahadi za nchi kwenye Jukwaa la kizazi chenye usawa, ambapo Tanzania ilijikita kushughulikia haki ya usawa wa kiuchumi.



ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT