Baada ya kupewa nafasi kidogo ya kutumbuiza na kuusalimu umma uliowasili katika kuupa nguvu uzinduzi wa uwanja wa Majaliwa hio jana Septemba 11,2022 Harmonize amewaahidi wadau wa Namungo FC kuwa atawapatia Zawadi ya wimbo kwajili yao. Uzinduzi huo uliambatana na mechi ambayo ilijumuisha klabu ya Namungo ilioikaribisha klabu ya Ruvu Shooting katika kushiriki mechi yao iliopangwa katika ratiba ya Michuano ya Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.