Iran imewahukumu adhabu ya kifo Wanaharakati wawili wa masuala ya mahusiano ya jinsia moja.
ADVERTISEMENT
Mahakama katika mji wa Urmia imewakuta na hatia Zahra Seddiqi Hamedani (31) na Elham Choubdar (24).
Waendesha Mashtaka wamewatuhumu wawili hao kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuhamasisha mahusiano ya jinsia moja na kuwasiliana na media zinazopingana na Jamhuri hiyo ya Kiislamu.
Chini ya sheria ya Iran, mahusiano ya jinsia moja ni kosa la jinai ambalo hukumu yake huanzia kwenye kuchapwa viboko hadi adhabu ya kifo.
ADVERTISEMENT