Rapa Dominique Armani Jones maarufu Lil Baby toka pande za Atlanta, Georgia, U.S ni rasmi atakuwa miongoni mwa watumbuizaji katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu itakayoanza Novemba 20, huko Qatar.
–
Lil Baby amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram pamoja na kudokeza Soundtrack ya “The World is Yours to Take” ambao ni miongoni mwa nyimbo zitakazotumika kwenye michuano hiyo.
–
Aidha, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa rapa huyo kushiriki katika shughuli za mpira akiwa kama mtumbuizaji.