Golikipa nambari moja Tanzania, Aishi Manura (Air Manula) anayedakia klabu ya Simba ameendelea kuwaacha midomo wazi wana Nyasa Big Bullets na Wadau wengine wa soka kwa namna anavyodaka vizuri mipira ya mashambulizi ya kushtukiza, kwa kuonesha umakini wa hali ya juu zaidi kama nafasi yake inavyotaka pale awapo katika mchezo. Hiyo imedhihirika kupitia mechi iliyochezwa ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba SC na wapinzani hao ambayo ilizaa mabao 2-0, ikileta matokeo jumuishi ya 4-0 kwa sababu klabu ya Simbahata ugenini ilipata kushinda goli 2-0.