ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Matumaini kwa Kinamama na Watoto Mkoani Tanga Baada ya Kupokea Msaada wa Vifaatiba Kutoka Taasisi ya Vodacom Tanzania

Tanga, Tanzania

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Sep 21, 2022
in BIASHARA
0
Matumaini kwa Kinamama na Watoto Mkoani Tanga Baada ya Kupokea Msaada wa Vifaatiba Kutoka Taasisi ya  Vodacom Tanzania
0
SHARES
100
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

May be an image of 6 people, people sitting, people standing and indoor

Vodacom Tanzania Foundation imetoa msaada wa vifaa tiba vya kitengo cha wagonjwa mahututi na wajawazito, vyenye thamani ya zaidi ya 130 milioni kwa hospitali za wilaya ya Kilindi na Handeni.
Taasisi imetoa msaada kwa mikoa 12 katika harakati za kupunguza vifo vya watoto wachanga tangu mwaka 2015.
Vodacom Tanzania pia imetambulisha mfumo wa m-mama mkoani Tanga ilikuokoa maisha ya kinamama wajawazito na watoto wachanga.17 Septemba 2022- Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaatiba vya watoto wachanga na uzazi katika hospitali za wilaya ya
Kilindi na Handeni mkoa wa Tanga ili kusaidia afya ya kinamama na watoto mkoani
humo.
Hospitali za wilaya ya Handeni na Kilindi zinahudumia takribani wanawake 2,600 kwa mwaka ambapo kati ya hao, wanawake 91 hujifungua kabla ya wakati. Msaada huu wa vifaatiba unalenga kuhudumia watoto njiti 300 kwa mwaka huku ukitoa msaada pia kwa wilaya jirani.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa taasisi ya VodacomTanzania Foundation Bi. Rosalynn Mworia alisema “Tunafuraha kuwepo hapa mkoani Tanga kutoa msaada huu muhimu ili kusaidia mipango ya afya ya uzazi kwa kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 110 milioni vitakavyosaidia kuokoa maisha ya watoto njiti wanaozaliwa mkoani hapa. Msaada huu
umeambatana na michango ya wafanyakazi wa Vodacom kupitia mpango wetu wa “Pamoja na Vodacom” ambapo wafanyakazi wa Vodacom hujitolea kusaidia jamii inayowazunguka na leo hii wametoa kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya kusaidi akina mama nawatoto wachanga.”
Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kuongeza oksijeni, vitanda vya joto, mashine za kupima mapigo ya moyo, mashine za ultrasound na vinginevyo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 110 milioni kwa hospitali mbili za wilaya hizo.
Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka watoto 15 milioni huzaliwa kabla ya wakati yaani njiti, kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania ambapo watoto 1 milioni hufariki kwa kukosa huduma muhimu. Kwa zaidi ya miaka kumi taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vifaa tiba katika vituo vya afya na hopsitali hapa nchini ili kuokoa maisha ya watoto njiti.
“Watoto njiti wana nafasi kubwa ya kukua na kuwa na afya nzuri bila ulemavu endapo watapata msaada wa vifaa na usimamizi wa afya kuzingatiwa na ndio maana tunaendelea kutoa msaada ili kuokoa maisha ya watoto njiti. Mpaka sasa katika juhudi zetu za kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga tumefikia mikoa 12 nchini Tanzania.

RelatedPosts

Digital Lending Executive Job Vacancy at Vodacom Tanzania Plc

Digital Lending Executive Job Vacancy at Vodacom Tanzania Plc

Jun 13, 2023

Vodacom Kuwapa Wasichana Fursa ya Kidigitali Nchini

Nov 16, 2022

Vodacom Tanzania yatoa msaada wa vifaa vya Tehama Jijini Dodoma

Nov 2, 2022
Load More

C2 General

Tunafuraha kutoa msaada kwenye huduma ya afya ya uzazi nchini kwa sababu hili ni eneo tunalohisi ni muhimu kwa maslahi ya taifa letu.” Aliongeza. Akipokea vifaa hivyo Mhe. Dk Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya alitoa shukrani zake kwa Vodacom Tanzania Foundation akisema kwamba msaada huo utasaidia
kwa kiasi kikubwa mkoa huo kufikia malengo yake ya afya ya watoto wachanga pamoja na wajawazito.
“Msaada huu umekuja muda muafaka ambapo serikali inashinikiza kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito. Vodacom imekuwa ikiongoza kwa kutumia teknolojia na mtandao wake kusaidia juhudi za serikali na hivi karibuni tumetambulisha huduma ya m-mama katika mkoa huu. Hivyo tunaamini tutafikia
lengo letu hivi karibuni” alisema. Kwa upande wake, Jonathan Bedenu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga alisema “Tunafuraha kupokea msaada huu na tunaimani utasaida watoa huduma kuokoa maisha ya watoto njiti na kuwapa nafasi ya kuishi maisha bora. Tutahakikisha kuwa vifaa vinatunzwa vizuri ili viweze kuhudumia watu wengi na kwa muda mrefu zaidi”

May be an image of 12 people, people standing and outdoors

May be an image of 8 people, people standing and outdoors

Related

Tags: VODACOM TANZANIA
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

BENKI YA NMB YAZINDUA HATI FUNGANI YA MUDA WA KATI
BIASHARA

BENKI YA NMB YAZINDUA HATI FUNGANI YA MUDA WA KATI

by SUZO SHUKRANI
Sep 25, 2023
Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
NMB BANK YAZINDUA NURU YANGU SCHOLARSHIP DIRISHA LA PILI
BIASHARA

NMB BANK YAZINDUA NURU YANGU SCHOLARSHIP DIRISHA LA PILI

by SUZO SHUKRANI
Sep 15, 2023
VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAWADHAMINI WAENDESHA BAISKELI WA TWENDE BUTIAMA
BIASHARA

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAWADHAMINI WAENDESHA BAISKELI WA TWENDE BUTIAMA

by SUZO SHUKRANI
Sep 13, 2023
MAVUNDE ABAINISHA DIRA SEKTA YA MADINI KUELEKEA 2030
BIASHARA

MAVUNDE ABAINISHA DIRA SEKTA YA MADINI KUELEKEA 2030

by SUZO SHUKRANI
Sep 12, 2023
TANZANIA, MAREKANI KUIMARISHA SEKTA YA MADINI NCHINI
BIASHARA

TANZANIA, MAREKANI KUIMARISHA SEKTA YA MADINI NCHINI

by SUZO SHUKRANI
Sep 8, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

September 2022
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930  
« Aug   Oct »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In