BINGWA wa mataji 15 ya dunia katika mchezo wa masumbwi duniani, FLOYD MAYWEATHER Jr, atarejea ulingoni jumapili hii, Septemba 25, kuvaana na mkali wa Mixed Marshall Arts (MMA), Mjapani MIKURU ASAKURA.
–
Pambano hilo litakalopigwa nchini Japan, linakuwa pambano la nne la maonesho (Exhibition bout), tangu FLOYD astaafu rasmi masumbwi ya ushindani mwaka 2017, kwa rekodi ya kushinda mapambo yote 50 aliocheza.
–
Pambano la kwanza alicheza mwaka 2018 dhidi ya mkali wa kick boxing, TENSHIN NASUKAWA, la pili mwaka 2020 dhidi ya LOGAN PAUL na la tatu mwaka 2022 dhidi ya DON MOORE na yote aliibuka mshindi
–
MAYWEATHER anaripotiwa kupiga pesa ndefu sana kupitia mapambano haya, hasa kwenye kutazama kwa kulipia (Pay per view ‘PPV).