Moto ambao Chanzo chake bado hakijafahamika umetekeza mabweni matatu ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Nyerere iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wanafunzi 107 wakinusurika na janga hilo
Moto huo umeteketeza madaftari ya wanafunzi, magodoro, mablanketi pamoja na vitu mbalimbali vilivyokuwa mabwenini jana Septemba 14, 2022.
“Nashangaa mwaka jana majira kama haya haya, mwezi huu huu shule iliungua jambo ambalo linaleta hofu kwetu kuwa ni imani za kishirikina” Severina Maluga mkuu wa shule
Aidha mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ameagiza kamati ya usalama wilaya ya mwanga kuweka shule hiyo kwenye uangalizi maalumu wa kiusalama ili kuepusha matukio hayo kujirudia.