Uwepo wa mradi wa kilimo cha zao la Vanilla visiwani Zanzibar (VANILLA VILLAGE) umedhihirisha kuongeza fursa za Ajira kwa wananchi ambao hapo awali hawakuwa na ajira ya kujipatia kipato kizuri cha kujikimu mahitaji yao muhimu ya kila siku kiasi hivyo imepelekea kukata wimbi la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana ambao huweza kuanza kujifunza matendo mabaya kama vile vitendo vya kiharifu na uvutaji bhangi ambayo unaleta athari kubwa ya kukosa nguvu kazi kitaifa. Mradi huo ulianzishwa chini ya Kampuni ya Vanilla Inernational Limited inayojihusisha na uwekezaji katika kilimo chake, na aina nyingine ya mazao kama parachichi, vitunguu swaumu, vitunguu maji, mapapai ikiongozwa na Mkurugenzi wake Simon Mkondya ambao kwa mara ya kwanza kabisa mradi huo umeanzishwa mkoani Njombe kwa kutambulishwa kama “VANILLA VILLAGE”.