Mtangazaji Mkongwe wa Shirika la Habari la CNN Christian Amanpour na Rais wa Iran Ebrahim Raisi walighairi na kukataa kufanya mahojiano baada ya kiongozi huyo kumtaka mtangazaji avae hijabu wakiwa jijini New York.
–
Amanpour ameeleza kuwa hakuna Rais yoyote wa zamani aliyewahi kumtaka afanye hivyo wanapokuwa nje ya Iran. Aidha alisema kuwa Msaidizi wa Rais alimwambia kuwa matakwa hayo yanatokana na hali inayoendelea nchini Iran hivi sasa.
–
Kifo cha Bi.Mahsa Amini (22) aliyekuwa anashikiliwa na polisi wa nidhamu nchini humo kwa kuvunja sheria za uvaaji hijabu kimeibua vurugu na maandamano makubwa.
Mahsa alipoteza fahamu na kufariki wiki iliyopita, masaa machache baada ya kukamatwa.