Imekuwa ni mara ya pili mfululizo Bondia Hassan Mwakinyo kutuma picha ilioandikwa MWAKINYO PROS, kwa mara ya kwanza Agosti 30,2022 aliituma akiambatanisha na maneno haya “Yupo muwezaji wa kila kilicho tushinda sisi …na kupitia yeye hakuna gumu wala kubwa kushinda yote..Akiamua” lakini leo hii ameambatanisha na kapsheni ikisema “Boxing academy coming soon” inayoonesha hivi karibuni anatarajia kuanzisha chuo cha mafunzo ya ngumi za kulipwa ili kuwapa fursa watanzania wengine kushiriki na kulipeleka taifa letu katika njia ya mafanikio zaidi.