Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo_ amethibitisha kuwa baada ya Promota Benjamin Shalom wa pambano lake dhidi ya Liam Smith kutoridhishwa na Refa kuonekana kutokuwa ‘fair’, sasa wamefikia makubaliano ya kurudiana na Liam Smith January 23, 2023.
–
Kupitia ukurasa wake Instagram. Mwakinyo ameandika:- .”kutokana na mchezo na kitendo cha Refa kuwa unfair kwangu kimemlazimu Promoter Benj Shalom kutupal nafasi ya re-match na Liam January 23″
–
Usiku wa Septemba 3 2022 Mwakinyo katika pambano dhidi ya Muingereza Liam Smith lililochezwa jijini Liverpool England alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano la round 12 ambalo hata hivyo lilikuwa gumzo kutokana na jinsi lilivyomalizika kwa utata.