
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ndugu Mohamed Abdalla amefungua Mkutano wa Usalama wa Huduma za Posta Barani Afrika unaoratibiwa na Umoja wa Posta Duniani (UPU) jijini Arusha, Jumatano tarehe 28 Septemba, 2022 katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU).
Mkutano huo umezileta pamoja nchi 46 wanachama wa PAPU ambapo Tanzania ni mwanachama na nchi mwenyeji wa Mkutano.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ni Msimamizi wa Huduma za Posta nchini, inashiriki Mkutano huo unaojadili usalama kwenye huduma zitolewazo na Mashirika ya Posta Afrika.

