Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeshtushwa na kasi ya kuvunjika kwa ndoa nchini chanzo kikubwa kikiwa ni kumomonyoka kwa maadili huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ndoa ni zaidi ya 300 zikivunjika kwa mwezi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, baada ya kukutana na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na makundi Maalum.
“Tumepata hesabu (ya ndoa kuvunjika) kwa mfano Dar es Salaam pekee yake zaidi ya ndoa 300 kwa mwezi zinavunjika. Hili tunaona ni tatizo kubwa ni janga. Sisi kama kamati tunaona haja kubwa ya kuishauri Serikali kuona jinsi gani kuchukua hatua kwa ajili ya kupambana na hali hii iliyopo,”amesema.
“Hili limeshamiri sana katika jamii yetu. Na kwakweli kuna haja ya Serikali kutafuta kwa kina chanzo nini na kuona ni hatua gani za kuchukua,” amesema.