Ng’ombe 12 wamepigwa na radi hadi kufa walipokuwa wakitolewa Malishoni Kijiji cha Mwingilo kata ya Ikungwigazi Wilayani Mbogwe Mkoani Geita
–
Akithibitisha kutokea kwa Tukio hilo Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikungwigazi Lenatus Mohalendi, amesema amepokea taarifa za kupigwa radi ng’ombe hao ambao walikuwa wanamilikiwa na Mfugaji mmoja anaejulikana kwa Majina ya John Elisha.
–
“Nimepigiwa simu mida ya Saa saba nadhani mida ya saa saba na nusu hivi nikapata taarifa kwamba kwenye kitongoji cha Malendi kwa Bwana John Elisha kuna tukio la radi ambapo ng’ombe wake 12 wamepigwa na wote wamefariki baada ya hapo nikaamua kufanya utaratibu wa kuwasiliana na polisi tukafika eneo la tukio, ” Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikungwigazi.
–
Bi. Katalina Elisha Fimbo ni Shangazi ake na John Elisha anasimulia tukio lilivyo kuwa ambapo amesema wakati tukio hilo linatokea alikuwa nyumbani kwake akimhudumia mgonjwa ndipo alipopata taarifa za Ng’ombe hao kupigwa na radi kutoka kwa Majirani.