Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal Anthony Stokes (34) anatafutwa na Polisi baada ya kutolewa kwa hati ya kumkamata kwa kushindwa kutokea Mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi yake.
–
Mshambuliaji huyo alishtakiwa na mpenzi wake wa zamani Eilidh Scott kwa kumsumbua kwa kumtumia meseji zenye matusi kupitia WhatsApp na barua pepe, ambazo zilikuwa zikifikia meseji 100 kwa siku.
–
Stokes alikiri makosa hayo, hata hivyo amekuwa hapokei simu za wafanyakazi wa ustawi wa jamii ambao wamekuwa wakijaribu kuandika ripoti kumhusu.