Padri mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi anadaiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto zaidi ya 10, ambao ni wanafunzi kuanzia darasa la sita hadi kidato cha kwanza waliokuwa wakihudhuria katika mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara.
–
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, zinadai kuwa baada ya wazazi, kubaini watoto wao kufanyiwa vitendo hivyo, walitoa taarifa hizo kwenye vyombo husika ikiwemo uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi na Polisi.
–
Jina la padri huyo na kituo chake cha kazi tunavihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili, inadaiwa, Padri huyo kila alipomaliza haja zake, aliwapa kila mmoja kati ya Shilingi 3, 000 na Shilingi 5,000.
–
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, akikataa kuthibitisha au kukanusha kukamatwa kwa padri huyo, Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kulaani kuwa “ni baya linalofedhehesha”.