Pipi zenye bangi zilizofungwa kama pipi za kampuni za Haribo na Skittles zimegundulika zikiuzwa na kuuziwa vijana na watoto nchini Uingereza.
–
Biashara ya pipi hizo imekuwa ikitangazwa wazi kabisa kupitia mitandao ya Tik Tok, Instagram, Facebook, Twitter, Snapchat,WhatsApp na Telegram.
–
Pipi hizo huambatana na dawa zingine za kulevya kama Heroin, Cocaine na Marijuana.
–
Kwa mujibu wa Polisi pipi hizo zimefungwa kwa rangi ya kuvutia vijana pamoja na watoto na hadi hivi sasa takribani watoto 6 wamefikishwa hospitali baada ya kutumia pipi hizo mmoja wao akiwa na umri wa miaka 8.
–
Watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na mtandao wa biashara hiyo haramu wengi wao wakiwa chini ya miaka 18.