Klabu ya Polisi Tanzania imegomea agizo la Bodi ya Ligi kuu la kutaka mchezo wao dhidi ya Coastal Union kuchezwa katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga na kusema mchezo huo utaendelea kuchezwa katika Uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID uliopo Mkoani ARUSHA kama ulivyopangwa awali kwa mujibu wa taratibu.
Kupitia barua yao kwa Bodi ya Ligi kuu, Polisi Tanzania imedai kuwa tayari wapo Arusha kwa maandalizi ya mchezo huo kwa uzingativu wa kanuni.
Awali Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilitoa taarifa kuwa mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga badala ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama ilivyokuwa awali.
Hii inakuja baada ya uwanja wa Mkwakwani kuthibitishwa kuendelea na matumizi baada ya ukaguzi uliofanywa na Kamati ya Leseni za klabu.