Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Masanja Kadogosa ameeleza kwamba shirika limekamilisha kuunganisha reli ya kisasa kutoka Dodoma mpaka Dar es salaam. Amesema hayo jana wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) walipofanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo.
Kadogosa amesema hii inakuwa ni kwa mara ya kwanza kufanya aina hiyo ya ukaguzi kwa kutumia treni ya Mkandarasi kwa kipande chote cha Dodoma hadi Dar es salaam moja kwa moja kwakuwa miundombinu ya reli kwa kipande hicho imeshakamilika.
Wabunge wametumia treni ya Mhandisi ya ukandarasi kwa njia ya reli ya kisasa kutoka Dodoma mpaka Dar es salaam huku wakiweka vituo katika baadhi ya maeneo kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi huo.