Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameitaka Serikali Kushughulikia vikundi vinavyofanya matukio ya Uhalifu ikiwemo “Panya Road” baada ya kukithiri kwa matukio yanayoathiri maisha ya watu na mali zao yanayofanywa na vikundi hivyo
Spika Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa viti maalum Mhe Bahati Ndingo kutoa hoja ya kuomba Bunge liahirishwe Kwa muda ili kujadili jambo hilo kama jambo la dharula linalosimama kwenye hoja ya usalama wa Raia na Mali zao
Hata hivyo spika wa bunge, alikataa ombi la Mbunge huyo na kusema kanuni ya Bunge ya 54 inatoa fursa kwa Mbunge kusimama na kueleza suala analotaka lijadiliwe na endapo Spika ataridhika atampa fursa ya kueleza na Kisha atatoa hoja ili Bunge wajadili lakini kwa mujibu wa kanuni ya 55 jambo hilo linapaswa kushughulikiwa na Serikali kwa utaratibu wa kawaida.
Hoja ya Mbunge imekuja siku moja baada kutokea kwa tukio la kikundi cha wahalifu kuvamia na kupora mali na fedha kujeruhi watu watatu na kusababisha kifo cha mtu mmoja katika eneo la Kawe Mzimuni manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.