Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa ameliagiza Baraza la Michezo Tanzania (BMT) pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukutana na kufanya tathmini mwenendo wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kutokana na matokeo yasiyoridhisha kisha kutoa ripoti ndani ya siku 14.
Pia ameiagiza BMT kufuatilia pambano la bondia Hassan Mwakinyo lililofanyika Uingereza Septemba 3 na Mwakinyo kupoteza kwa TKO raundi ya nne dhidi ya Liam Smith.
Credit : Mwanaspoti_