Manchester United iko tayari kuanza mazungumzo na mshambuliaji muingereza Marcus Rashford, 24, kuhusu mkataba mpya baada ya kuonyesha kiwango kizuri tangu kuanza kwa msimu huu. (Sun)
Juventus inataka kubadilishana wachezaji ikimtaka kiungo wa Aston Villa mbrazil Douglas Luiz, na kumtoa mshambuliaji muitalia kwenda Villa, Moise Kean, 22. (JuveLive, via HITC)
Luiz anatarajia kuondoka kama mchezaji huru dirisha lijalo mkataba wake utakapomalizika. (UOL, via Sun)
Galatasaray imekubali kumchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja mshambuliaji wa Paris St-Germain Muargentina Mauro Icardi, 29. (Fabrizio Romano)

CHANZO CHA PICHA,HUW EVANS PICTURE AGENCY
Kiungo wa zamani wa Manchester United na Hispania Juan Mata, 34, pia anatarajia kujiunga Galatasaray. (Ali Naci Kucuk)
Thomas Tuchel ameshangazwa na kutimuliwa kwake Chelsea na aliwaomba mabosi wa klabu hiyo kumpa angalau nafasi nyingine na muda zaidi waligoma. (Sun)
Barcelona imekanusha kukataa ofa ya kununua hisa za Barca Studios iliyotolewa na mlinzi wake wa zamani Gerard Pique, 35. (ESPN)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Everton haionekani kama itasajili golikipa aliye huru kufuatia kuumia kwa kipa wake wa England Jordan Pickford, 28, katika debi ya Merseyside, maumivu yatakayomuweka nje kwa mwezi mzima (Sky Sports)
Winga wa Southampton Nathan Redmond, 28 anajiandaa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya dirisha la usajili la Uturuki kufungwa leo alhamisi. (Turkish Football, via Hampshire Live)
Shakhtar Donetsk wanataka zaidi ya £30m kwa ajili ya winga wake wa Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21, kufuatia kusakwa na vilabu vya Everton na Arsenal. (Gianluca di Marzio, via HITC)