Liverpool wanaongoza katika kinyang’anyiro cha mbele ya Manchester United kumpata kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19.(Telegraph – subscription required)
Hata hivyo, Liverpool wanafikiria kumnunua kiungo wa Wolves na Ureno Matheus Nunes, 24, kama mbadala wa Bellingham. (UOL, via Mirror)
Winga wa Chelsea Hakim Ziyech, 29, alikuwa na nia ya kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto huku klabu za zamani za Ajax na AC Milan zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco. (Football.London)
Chelsea walimtafuta mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, wakati wa dirisha la kiangazi, kulingana na mkurugenzi wa klabu hiyo Paolo Maldini. (FourFourTwo)
Mkurugenzi wa michezo wa Red Bull Salzburg Christoph Freund amekataa kufutilia mbali uwezekano wa kujiunga na Chelsea katika jukumu kama hilo, na kusema The Blues walionyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Austria na Slovenia Benjamin Sesko, 19, wakati wa majira ya joto. (Sky Austria, via 90 Min)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Brighton Moises Caicedo, 20, anasema analenga kuchezea klabu ya pwani ya kusini na Ecuador kwenye Kombe la Dunia la 2022 lakini “hakuna mtu ambaye angekataa ofa kutoka kwa Chelsea au klabu nyingine yoyote kama hiyo” (Ole, via 90 Min)
Newcastle United wanavutiwa na winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Arsenal na Brentford. (Football Insider)
Shakhtar Donetsk wamethibitisha kukataa ombi la Everton la euro milioni 30 kwa ajili ya Mudryk. (90min)
Valencia, Villarreal, Celta Vigo na Real Sociedad wanapanga ofa za kabla ya mkataba wa awali kwa mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile Ben Brereton Diaz, huku Everton na Leeds pia zikimlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Meneja wa Ufaransa Didier Deschamps anasema hatamchagua kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba, ambaye anakabiliwa na jeraha la goti, katika kikosi chake cha Kombe la Dunia 2022 hadi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atakapokuwa sawa kabisa. (Mirror)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag atapewa takriban pauni milioni 70 za kutumia katika dirisha la usajili la Januari na kiasi hicho kinaweza kuongezeka iwapo mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, ataondoka Old Trafford. (Sun)
Mlinzi wa zamani wa Tottenham na England Danny Rose, 32, anakaribia kusajiliwa na klabu ya Ugiriki AEK Athens kama mchezaji huru baada ya kuondoka Watford mapema mwezi huu. (Sun)
Brighton wanaendelea na mazungumzo na meneja wa zamani wa Shakhtar Donetsk Roberto de Zerbi huku wakitafuta kuchukua nafasi ya Graham Potter. (Calciomercato – kwa KiitalianoJuventus pia inaweza kuwa chaguo kwa De Zerbi ikiwa timu hiyo ya Serie A itaamua kuachana na meneja Massimiliano Allegri. . (Sportmediaset, via Football Italia)
Kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea, 31, anasema alikuwa karibu kujiunga na Wigan mwaka wa 2009, kabla ya kuhamia Old Trafford. (BT Sport, via Mail)